 |
Idara ya sanaa chuo kikuu Dar es salaam chimbuko la vipa | ji |
Na Timothy Mwakimbwala
Anajulikana kama Ujio Netho wengi wanamfaamu kama Ujio ndio jina alilozoea kulitumia kwenye tamthilia mbalimabali alizocheza. Ni msanii ambaye ameibuka kwa kasi ya ajabu kwenye tasnia ya uigizaji bongo. Nafasi anazopendelea kucheza ni za uchekeshaji ambazo anaonekana kuzimudu kwa kiwango cha juu. Ujio ni msanii toka kundi kongwe la sanaa nchini linajulikana kama Kaole sanaa group ambalo limewatoa mastaa kibao wanaofanya vema kwenye kiwanda cha filamu bongo kama Ray, kanumba , Johari, Tino, tea na wakali wengine kibao
 |
Ujio netho |
Unapomkuta nje ya fani ya uigizaji ni mtu mmoja mpole ambaye bila kuwahi kumuona unapoambiwa habari zake huwezi kuamini. Lakini ukweli ni kwamba huyo ndio Ujio Netho kijana mwenye vituko kupitiliza awapo kazini. Ujio kwa sasa anamalizia mwaka wake wa tatu katika chuo kikuu cha Dar es salaam ambapo alijiunga toka mwaka 2009 ili kukiendeleza kipaji chake cha uchekeshaji.
 |
Ujio Netho akiwa na Bambo mkongwe wa comedy zao kutoka kaole sanaa group |
 |
ujio Netho katika pozi |
No comments:
Post a Comment