Thursday, September 29, 2011

MKALI WA COMEDY ALIYETOKA KAOLE ARTS GROUP MPAKA FPA UDSM

Idara ya sanaa chuo kikuu Dar es salaam chimbuko la vipaji


Na Timothy Mwakimbwala
Anajulikana kama Ujio Netho wengi wanamfaamu kama Ujio ndio jina alilozoea kulitumia kwenye tamthilia mbalimabali alizocheza. Ni msanii ambaye ameibuka kwa kasi ya ajabu kwenye tasnia ya uigizaji bongo. Nafasi anazopendelea kucheza ni za uchekeshaji ambazo anaonekana kuzimudu kwa kiwango cha juu. Ujio ni msanii toka kundi kongwe la sanaa nchini linajulikana kama Kaole sanaa group ambalo limewatoa mastaa kibao wanaofanya vema kwenye kiwanda cha filamu bongo kama Ray, kanumba , Johari, Tino, tea na wakali wengine kibao

Ujio netho
Unapomkuta nje ya fani ya uigizaji ni mtu mmoja mpole ambaye bila kuwahi kumuona unapoambiwa habari zake huwezi kuamini. Lakini ukweli ni kwamba huyo ndio Ujio Netho kijana mwenye vituko kupitiliza awapo kazini. Ujio kwa sasa anamalizia mwaka wake wa tatu katika chuo kikuu cha Dar es salaam ambapo alijiunga toka mwaka 2009 ili kukiendeleza kipaji chake cha uchekeshaji.
Ujio Netho akiwa na Bambo mkongwe wa comedy zao kutoka kaole sanaa group
ujio Netho katika pozi

Saturday, September 24, 2011

BIG SHAH A.K.A THE BIG PRODUCER MKALI WA MUZIKI TOKA FPA (UDSM) ALIYEANGUKIA KWENYE BONGO MOVIES

Na Timothy Mwakimbwala
Anajulikana kama Big Shah kutokana na kuwa na mwili mkubwa ni mzaliwa wa Dar es salaam. Ni kijana aliyebalikiwa kuwa na vipaji vingi. Mwaka 2008 akitokea Shule alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es salaam akitafuta shahada ya sanaa (Fine & Peforming Arts), akitaka kukiendeleza kipaji chake cha Utengenezaji Muziki (Producer). Big Shah ameshawahi kuwatoa wasanii chipukizi kibao akiwemo Richard Nyandindi na wengineo wakati huo akiwa producer jijini Mbeya.
.
Big Shah akiwa darasa la Muziki FPA akipiga saxaphone

Big Shah akiwa katika darasa la muziki FPA (UDSM) akijifunza kupiga gitaa. By Timothy Mwakimbwala
Big Shah akiwa studio akitengeneza Muziki

 Big shah kwa sasa amemaliza shahada yake ya kwanza ya sanaa (BA in Fine & Performing Arts) katika chuo kikuu cha Dar es salaam. Pamoja na ugalacha wake wote kwenye tasnia ya muziki aliamua kuweka mikoba pembeni kidogo na kujiingiza kwenye Bongo Movies ambapo kwa sasa ameamua kufungua kampuni yake inayojulikana kama  Natives Filmes.

Big Shah akiwa na camera akishoot  Documentary
Big Shah aliyeshika camera akiwa mzigoni kushoot filamu
Huyu ndio Big Shah mkali wa Muziki  toka kiwanda cha vipaji FPA anayetingisha ndani ya Bongo Movies akiwa mzigoni kwenye kutengeneza filamu. By Timothy Mwakimbwala

Friday, September 23, 2011

RICHARD NYANDINDI MGODI MPYA WA HIP HOP TOKA FPA (UDSM) UNAOTEMA MAWE KWA KASI NDANI YA ULIMWENGU WA HIP HOP BONGO

Na Timothy Mwakimbwala.

Anaitwa Richard Nyandindi mzaliwa wa Dar es salaam. Ni mkali wa michano anayeusudu MIC kuliko kitu chochote. Alianza kujulikana kwa kupanda kwenye maconcert wakati huo akiwa anasoma Mbalizi sec school iliyoko Mbeya.Kwa kuwa sanaa ipo damuni aliamua kujiunga chuo kikuu cha Dar er salaam ili kusomea shahada ya sanaa (Fine & Performing Arts) akifuata nyayo za aliyekuwa Producer wake wakati huo akitokea Mbeya, hapa namamzungumzia Big Shah.

Richard Nyandindi kwa sasa yuko mbioni kuachia kibao chake kipya kinachoitwa ABC akimshirikisha wa jina wake Philipo Nyandindi O-TEN. Wapenzi wa Hip Hiop kaeni mkao wa kula kusikiliza ngoma kali ya Richard Nyandindi
                                               Richard Nyandindi akiwa katika pozi toauti.

The former Producer wa Richard Nyandindi Big Shah a.k.a Shah Native the big producer akiwa mtamboni. Photo by Timothy Mwakimbwala.

Friday, September 16, 2011

EVA CHARLES KALUNDE ALMASI ILIYOJIFICHA MCHANGANI..........!

 Na Timothy A. Mwakimbwala.
Anaitwa Eva Charles Kalunde ni mzaliwa wa Tabora.Ni lulu mpya kwenye tasnia ya muziki was Injili. Mbio zake za usanii zilianza kukomaa alipokuwa sekondari. Wakati huo akiwa anasoma shule ya sekondari Mwinyi iliyopo Tabora mjini. Alianza kujulikana kwa kuimba kwenye makutano ya wanafunzi maarufu kama "joint mass" zinazowakutanisha wanafunzi wa shule mbalimbali za Tabora. Hapo ndipo alipokutana na wanafunzi wenzake Mariam Joseph Kariuk na Martha Tiluli ambapo kwa pamoja waliamua kuanzisha band iliyojulikana kama Doxa Band.

Baada ya kuanzisha band hiyo ndipo walipoamua kumtafuta mlezi ambapo kwa pamoja waliamua kujiunga na kanisa TAG Maranatha Miracle Centre lililopo Cheyo B Tabora mjini chini ya Mchungaji Lutengano Mwasongela ambaye aliamua kuubeba mzigo huo na kuwa mlezi wao.
Eva Charles ni almasi iliyojificha kwa sababu si kitu cha kawaida kwa mtu mwenye kipaji cha kweli kama cha Eva kutovuma angalau tu kwa mkoa wa Tabora. Mara ya kwanza nilipomuona akiimba pamoja na band yao katika kanisa a TAG Maranatha Miracle Centre haikuwa rahisi kuamini kwamba nyimbo walizokua wanaimba ilikuwa ni live band. Kwani waliimba nyimbo zao kwa ustadi mkubwa kana kwamba walikuwa wanatumia back up CD. Na haikuwa rahisi kuamini kwamba hawakuwahi kurekodi hata albamu moja.

Eva Charles kwa sasa amemaliza kidato cha sita katika shule ya sekondari Uyui iliyopo pia Tabora mjini. Ndoto zake kimaisha ni siku moja kuwa msanii wa kimataifa wa muziki wa Injili na kuwa msomi mkubwa. Ili kutimiza hilo kwa sasa anatarajia kujiunga na chuo kikuu kwa mwaka wa masomo 2011/2012 kwa ajili ya kuitafuta shahada yake ya kwanza.
                            Huyu ndio Eva Charles Kalunde zao kutoka TAG Maranatha Miracle Centre lilopo Cheyo B (Tabora mjini) kwa Mchungaji kiongozi Mchungaji Lutengano Mwasongela.

Saturday, September 10, 2011

TAG MARANATHA MIRACLE CENTRE "Cheyo B" Tabora Mjini

Mchungaji kionngozi wa kanisa la TAG Maranatha Miracle Centre lililopo Cheyo B karibu na shule ya msingi Cheyo B (Tabora Mjini), Pastor Lutengano Mwasongela anapenda kuwakaribisha kwenye Ibada ya Miujiza inayofanyika kila jumapili kuanzia saa 3 asubuhi na kuendelea. Na kwa huduma ya maombezi na ushauri Mchungaji kiongozi na jopo lake la wachungaji anapatikana kila siku ofisini kwake kanisani hapo kuanzia saa 3 hadi saa 12 jioni. mnakaribishwa wakazi wote wa Tabora na vitongoji vyake.

Wednesday, September 7, 2011

BREAKING NEWZ

TIMOTHY MWAKIMBWALA MWASISI WA BLOG HII
www.timothymwakimbwala.blogspot.com NI BLOG AMBAYO IMEASISIWA NA TIMOTHY A. MWAKIMBWALA AMBAYE  KWA SASA AMEAJIRIWA KAMA PROJECT DIRECTOR  COMPASSION INERNATIONAL TANZANIA - TABORA. LENGO LIKIWA NI KUKUPA HABARI MBALIMBALI ZA KIJAMII, MICHEZO NA BURUDANI.