Mchugaji Musa |
One 2 one Interview by Timothy Mwakimbwala.
Mwandishi: Bwana asifiwe Mchungaji, za uzima?
Mchungaji: Amina, tunamshukuru Mungu kwa kuwa wazima wa afya maana kuna wengi walitamani kuwepo leo lakini hawakuweza kuamka.
Mwandishi: Mchungaji naweza kujua historia yako kwa ufupi?
Mchungaji: kwa jina naitwa Mchungaji Musa Sheka Makala natambulika zaidi kama askari kutoka jeshi la serikali ya mbinguni kikosi cha mizinga. Nilizaliwa mwaka 1982 mkoa wa Singida wilayani Iramba katika kijii cha Makunda.
Mwandishi: Asante sana kwa historia yako sasa ilikuwajekuwaje mpaka ukajikuta umeajiliwa kama askari wa jeshi la serikali ya mbinguni katika kikosi cha mizinga?
Mchungaji: (Anacheka kidogo) Mnamo mwaka 2005 nilisikia mungu akisema nami nikiwa Igunga mkoani Tabora. Ikatokea katika kanisa nililokuwa nasali alikumja Mchungaji kutoka Dar es salaam Mchungaji Martin kuhudumu kwenye semina baada ya semina kumalizika aliniomba twende wote Dar es salaam. Huko nilianza kwa kuombea wagonjwa mahospitalini hasa hospitali ya Taifa ya Muhimbili na nikaanza kujifunza kuhuburi chini ya mwalimu wangu mchungaji Martini. Mnamo 2006 nikaenda kufungua kanisa moshi mkoani Kilimanjaro. Ki ukweli huko nilimuona Mungu kwani kwa siku ya kwanza tu niliweza kupata washirika 35. Huko nilidumu kwa mwaka mmoja na ilipofika 2007 nikarudi tena Dar es salaam kuendelea na huduma. Nilipofika Dar es salaam safari hii nikaanza kupata mihaliko ya mikutano na semina toka sehemu mbalimbali za Tanzania.
Mwandishi: Katika huduma yako ulishawahi kuifikia mikoa ipi?
Mchungaji: Mpaka sasa nimeshatembelea Dar es salaam, Kilimanjaro, Arusha, Singida, Shinyanga, Mwanza, Dodoma, Mtwara, Lindi, Tanga na Tabora.
Mwandishi: Ilikuwajekuwaje mpaka ukaamua kuweka kambi Tabora?
Mchungaji: Mtumishi wa Mungu Mchungaji Lutengano Mwasongela baada ya kusikia habari zangu aliamua kunitafuta na kuniomba nije kuwa mchungaji mzaidizi katika kanisa lake lililo chini ya TAG, linalojulikana kama TAG Maranatha Miracle Centre lililopopo Cheyo B Tabora mjini. Nakumbuka hiyo ilikuwa 2010 mwezi wa nne ndipo nilipofika hapa na ndipo napohudumu mpaka sasa.
Mwandishi: Ni mtumishi gani unayempenda hapa Tanzania na ungependa kuwapa ushauri gani watumishi wa Mungu?
Mchungaji: Kiukweli mimi nampenda sana Mwalimu Mwakasege jinsi anavyofundisha. Cha kuwashauri watumishi wa Mungu ambao Mungu amewaita wanatakiwa wakae chini ya Mungu na kumsikiliza roho wa Mungu awape cha kusema katika ulimwengu wa sasa na ndipo watakapoinuliwa kwenda viwango vingine.
Mwandishi: Asante sana mchungaji kwa ushirikiano wako uliouonyesha na Mungu akubariki sana.
Mchungaji: Amina, nashukuru sana na karibu tena siku nyingine ukiwa na lolote Mungu akubariki sana.
Mchungaji Musa akiwa ofisini |
Huyu ndio Mchungaji Musa ambaye anahubiri kila jumamosi saa 2:30 Usiku katika kipndi cha Usilie tena C.G fm. Ukiwa na shida za Maombezi na Ushauri Mchungaji Musa pamoja na Mchungaji kiongozi Mchungaji Lutengano Mwasongela wanapatikana ofisini katika kanisa la TAG Maranatha Miracle Centre lililopo Cheyo B Tabora Mjini kila siku kuanzia Jumatatu hadi Jumamosi saa 4 hadi saa 12 jioni.
Kwa mawasiliano piga: 0788-495870
0762-111492
0652-364772
Mchungaji musa akiwa ofisini |
Mchungaji Musa akiwa na Eliud Moses Mhasibu wa Compassion |